Johari RotanaDAR ES SALAAMRRRRR
OVERVIEWACCOMMODATIONDININGMEETINGS & EVENTSWEDDINGSRECREATIONOFFERSREVIEWSGALLERY
VYAKULA & BURUDANI

Sehemu mpya kabisa ya kula chakula jijini Dar es Salaam, inawapatia wageni wa hotelini na wakazi wa Jiji uzoefu wa kipekee wa uaandaaji wa chakula usioweza kusahaulika. Sehemu zetu nne za kitofuati zinakupeleke katika safari ya kipekee ya mapishi, kuanzia mapishi halisi ya Kichina ukiwa Noble House hadi kwenye bufee kubwa ya ladha za Kimediterania, Kihindi Kiarabu na Kiswahili ukiwa katika mgahawa wa siku nzima wa Zafarani. Kibo Lobby Lounge ni sehemu ya kufurahia kahawa yako au kinywaji cha starehe, huku Hamilton’s Gastropub ni kituo cha starehe kilichochangamka ambacho kitakuvutia kwa vyakula vya Kiingereza na Kimarekani.

Find all of the latest offers and promotions across our Restaurants on our pages at Rotana Times ]
HAMILTON’S GASTROPUB
Mapishi ya Kiuingereza na Kimarekani

VIEW PHOTOS
VIEW MENU
VIEW OFFERS
BOOK A TABLE

Ufanye usiku wako uwe wa kukumbuka ukiwa Hamilton’s Gastropub mahali ambapo mapishi ni matamu na mazingira yanachangamsha. Menyu ya kuvutia ya vyakula vya Kiuingereza na Kimarekani vinatengenezwa kwa bashasha katika eneo hili lililochangamka kwa mapambo ya mtindo wa zama za kikoloni, viti vya kukaa vya nje na ndani na samani za kustarehesha.

Furahia muziki murua na vinywaji vinavyoandaliwa na kumiminwa kitaalamu katika baa hii ya kipekee Jijini Dar es Salaam inayokuhakikishia nyakati za furaha na chakula kizuri kuanzia mchana hadi usiku.

Eneo la kucheza watoto lililopo karibu na Hamilton's, linakuwezesha kustarehe na kufurahia kinywaji au mlo wakati watoto wako wanafurahia michezo.

Opening Hours:
5.00 pm – 12 am

NOBLE HOUSE
Mapishi ya Kichina

VIEW PHOTOS
VIEW MENU
VIEW OFFERS

Kufunguliwa hivi karibuni

Furahia ladha halisi ya nchi za Mashariki ukiwa kwenye mgahawa wetu mahususi wa vyakula vya Kichina, Noble House; mahali ambapo wapishi wetu wa Kichina wamechagua aina mbalimbali ya vyakula halisi vyenye ladha nzuri ambazo zitakupeleka China bila kutoka Tanzania. Ukiwa na samani za kisasa, mwanga mtulivu na mapambo ya kupendeza ambayo yanaakisi ustadi wa kipekee na haiba ya Mashariki ya Mbali, unaweza kula chakula cha kipekee cha jioni ukiwa na familia, marafiki au wafanyakazi wenzako katika eneo hili mwandani la kulia chakula.

Opening Hours:
6.00 pm – 11.00 pm

ZAFARANI ALL DAY DINING
Mapishi ya Kimediterania, Kihindi Kiarabu na Kiswahili

VIEW PHOTOS
VIEW MENU
VIEW OFFERS
BOOK A TABLE

Una uchaguzi mwingi wa vyakula ukiwa Zafarani, mgahawa wetu wa kisasa wa siku nzima ambapo wapishi wetu wenye vipaji vya hali ya juu wanaandaa vyakula vinavyovutia na mapishi ya Kimediterania, Kihindi, Kiarabu na Kiswahili. Wageni wanaweza kujaribu ladha za vyakula kutoka duniani kote wakati wa kifungua kinywa, chakula cha mchana na cha jioni katika eneo hili la kustarehesha lenye mwanga mtulivu. Chagua kutoka kwenye bufee kubwa au chagua chakula unachokipenda kutoka kwenye menyu yetu ya a la carte.

Opening Hours:
Kifungua Kinywa: 6.30 am – 10.30 am
Chakula cha Mchana: 12:00 pm - 2:30 pm
Chakula cha Jioni: 6:00 pm - 10:00 pm

KIBO LOBBY LOUNGE
Vinywaji, vyakula vyepesi, vitobosha na vitindamlo

VIEW PHOTOS
VIEW MENU
VIEW OFFERS

Kaa kwenye kiti na tazama dunia ikiendelea ukiwa Kibo Lobby Lounge, sehemu iliyotengenezwa kifahari ikiwa na mwanga tulivu na mapambo ya kisasa. Panafaa kwa mikutano isiyo rasmi na wafanyakazi wenzako au wateja wako au kwa mikutano na marafiki au familia mkiburudika na chai au kahawa na vitobosha. Mgahawa wetu unakupatia maeneo kadhaa ya kukaa yenye faragha ambapo unaweza kufanya mazungumzo au mikutano ya kawaida. Vitindamlo vitamu, vyakula vyepesi, na vinywaji vinavyoburudisha pia vinapatikana kwenye menyu inayotamanisha.

Opening Hours:
7.00 am – 11.00 pm

HUDUMA YA CHAKULA CHUMBANI
Mapishi ya Kimataifa

VIEW PHOTOS
VIEW MENU

Wageni wanaweza kufurahia mapishi yanayoandaliwa Johari Rotana huku wakiwa chumbani mwao, kwenye suite au chumba cha kupanga, kwa kuchagua miongoni mwa mapishi mbalimbali ya kimataifa kutoka kwenye menyu yetu ya huduma ya chakula chumbani.

Kuanzia kitafunio au kiburudisho cha usiku wa manane hadi mlo binafsi ukijumuika pamoja na marafiki na familia, tunaweza kukuandalia vyakula unavyovipenda na kukuletea chumbani kwako. Wewe tupigie tu simu na tutafurahia kukusaidia.

Opening Hours:
Saa 24 kila siku, siku 7 za wiki

THE CIGAR LOUNGE
Classic British

VIEW PHOTOS

Ukumbi wa Cigar wa kifahari ulioundwa kwa ajili ya wapenzi wa Cigar kufurahia mchanganyiko bora katika mazingira yenye utulivu na staha.

Opening Hours:
Jumatatu -Jumapili: 4:00 PM - 1:00 AM

ABOUT ROTANAROTANA WEBSITES
HISTORY
ROTANA VALUES
VISION / BRAND PROMISE
OUR AWARDS
BOARD OF DIRECTORS
CORPORATE EXECUTIVES
HOTEL DEVELOPMENT
UPCOMING OPENINGS
BRANDMARK
INDUSTRY PARTNERS
ROTANA EARTH / CSR
NEWS ROOM
PRESS & MEDIA
MEDIA LIBRARY
SALES OFFICES & GDS
CORPORATE GUESTS
www.rotana.com
www.rotanatimes.com
www.rotanaearth.com
www.rotanacareers.com
www.rotanalifestyle.com
© Copyright 2024 Rotana Hotel Management Corporation PJSC.
Please see our
Terms of Use
Privacy Policy
Cookie Settings
This website uses cookies so that we can improve your user experience and measure the performance of our site.
If you continue on this website, you will be providing your consent to our use of cookies.
Read our Cookie Statement
ACCEPT